Deuteronomy 30:1-6

Mafanikio Baada Ya Kumgeukia Bwana

1 aWakati baraka hizi zote pamoja na laana nilizoziweka mbele yako zitakapokujia, nawe ukazitafakari moyoni popote Bwana Mwenyezi Mungu wako atakapokutawanya miongoni mwa mataifa, 2 bhapo wewe na watoto wako mtakapomrudia Bwana Mwenyezi Mungu wako, na kumtii kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote kulingana na kila kitu ninachokuamuru leo, 3 cndipo Bwana Mwenyezi Mungu wako atakapokurudisha kutoka utumwani na kukuhurumia, naye atakukusanya tena kutoka mataifa yote kule alikutawanya. 4 dHata kama umefukuziwa katika nchi ya mbali kiasi gani chini ya mbingu, kutoka huko Bwana Mwenyezi Mungu wako atakukusanya na kukurudisha. 5 eYeye Bwana atakurudisha katika nchi iliyokuwa mali ya baba zako, nawe utaimiliki. Naye atakufanya ufanikiwe sana na kukuzidisha kwa idadi kuliko baba zako. 6 f Bwana Mwenyezi Mungu wako ataitahiri mioyo yenu na mioyo ya wazao wenu ili mweze kumpenda kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote ukaishi.
Copyright information for SwhKC